Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Historia

Chimbuko    la    Ofisi    ya    Makamu    wa    Pili    wa    Rais    Zanzibar limeanzia  kutokana  Mabadiliko  ya  Kumi  ya  Katiba  ya  Zanzibar ya   1984,   Toleo   la   mwaka   2010,   Kifungu   cha   39[1]).   Kifungu hicho  kimeanzisha  nafasi  za  Makamu  wa  Kwanza  wa  Rais  na Makamu  wa  Pili  wa  Rais  wa  Zanzibar  ambapo  Makamu  wa  Pili wa  Rais  amepewa  jukumu  la  kuratibu  shughuli  zote  za  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ofisi  ya  Makamu  wa  Pili  wa  Rais  ni  taasisi  ya  Serikali  ambayo kabla  ya  mabadiliko  hayo  ya  Katiba  ilikuwa  ikijulikana  kwa  jina la Afisi ya Waziri  Kiongozi  ambaye jukumu lake kuu ni kuratibu shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.