Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini Mchango wa Mashirika ya Serikali na Binafsi katika Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi Katika kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa maendeleo ya Zanzibar.
Mhe. Hemed ameeleza hayo katika Hafla ya Uchangiaji wa Rasilimali za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutambua umuhimu wa Mashirika hayo kwa kuwashirikisha moja kwa moja katika Suala la uchangiaji wa Rasilimali za kufanikisha Zoezi hilo