Lengo la OMPR : Lengo la kuanzishwa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais ni kuratibu na kusimamia shughuli zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na zile za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazohusiana na masuala ya Muungano.
Majukumu ya OMPR
a. Kutoa huduma kwa Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais katika ofisi na makaazi yake;
b. Kuratibu shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mambo ya Muungano ambayo yanajumuisha:
- Kuhakikisha kwamba Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinatoa huduma bora kwa umma;
- Kusimamia miradi yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano inayotekelezwa Zanzibar;
- Kusimamia kazi za Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zinazofanya shughuli zake Zanzibar;
- Kuratibu shughuli za kukabiliana na maafa kwa kuweka mifumo imara ya kujikinga, kujiandaa na kukabiliana na majanga kabla, wakati na baada ya kutokea;
- Kuratibu sherehe na maadhimisho ya kitaifa pamoja na shughuli za kuwaenzi viongozi wa kitaifa kama ilivyoelekezwa katika Sheria Namba 5 ya 2019;
c. Kusimamia kazi za Baraza la Wawakilishi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.