Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameshiriki katika Uzinduzi wa Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyozinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.

